Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Maendeleo katika Uswedi

  Katika Uswedi vilevile vijana kutoka Wittenberg wakachukua maji ya uzima kwa watu wa kwao. Waongozi wawili wa Matengenezo katika Swede, Olaf na Laurentius Petri, walijifunza chini ya Luther na Melanchton. Kama mtengenezaji mkuu, Olaf akaamsha watu kwa ufundi wake wa kusema, hivyo Laurentius, sawasawa na Melanchton, alikuwa na uangalifu na utulivu. Wote wawili walikuwa na uhodari imara. Mapadri wakikatoliki wakasukuma watu wajinga na wa ibada ya sanamu kwa nyakati nyingi. Olaf Petri kwa shida akaokoka na maisha yake. Watengenezaji hawa walikuwa, basi, wakilindwa na mfalme, aliyekusudia juu ya Matengenezo na akakaribisha hawa wasaidizi hodari katika vita ya kupinga Roma.TSHM 112.4

  Mbele ya mfalme na watu waliojifunza wa Swede, Olaf Petri kwa uwezo mkubwa akatetea imani ya matengenezo. Akatangaza kwamba mafundisho ya mababa yanapaswa kukubaliwa tu kama yakipatana na Maandiko; akatangaza kwamba mafundisho mhimu ya imani yanayofundishwa katika Biblia kwa hali ya wazi ili wote waweza kuyafahamu.TSHM 113.1

  Shindano hili linaonyesha watu wa namna gani wanaokuwa katika jeshi la Watengenezaji. Hawakuwa wajinga, watu wa kujitenga, wenye mabishano wa fujo--mbali ya ile. Walikuwa watu waliojifunza Neno la Mungu na waliojua vizuri kutumia silaha walizozipata kwa gala ya silaha ya Biblia. (Walikuwa) wanafunzi na wanafunzi wa elimu ya tabia na sifa za Mungu na dini (Theologie), watu wakamilifu waliozoea mambo ya ukweli wa injili, na walioshinda kwa urahisi wenye kutumia maneno ya ovyo ya uongo wa vyuo na wakuu wa Roma.”TSHM 113.2

  Mfalme wa Swede akakubali imani ya Waprotestanti, na baraza la taifa likatangaza ukubali wake. Kwa matakwa ya mfalme ndugu hawa wawili wakaanza utafsiri wa Biblia nzima. Ikaagizwa na baraza kwamba po pote katika ufalme, wachungaji walipashwa kueleza Maandiko, na kwamba watoto katika vyuo walipashwa kufundishwa kusoma Biblia.TSHM 113.3

  Walipookoka na magandamizo ya Roma, watu wa taifa la Uswedi wakafikia hali ya nguvu na ukubwa wasiofikia mbele. Baada ya karne moja, taifa hili ndogo na zaifu likawa la kwanza katika Ulaya lililosubutu kutoa mkono wa usaada--kwa ukombozi wa Ujermani mda wa shindano ndefu la Vita ya miaka makumi tatu. Ulaya yote ya Kaskazini ilionekana kuwa tena chini ya ukorofi wa Roma. Majeshi ya Swede ndiyo yaliwezesha Ujeremani kupata uhuru wa dini kwa ajili ya Waprotestanti na kurudisha uhuru wa zamiri kwa inchi zile ambazo zilikubali Matengenezo.TSHM 113.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents