Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Uharibifu wa Hekalu Tukufu

    Siku mbili kabla ya Pasaka, Kristo akaenda tena na wanafunzi wake kwa mlima wa Mizeituni kutazama mji. Mara moja tena akatazama hekalu katika fahari ya kungaa kwake, taji la uzuri. Solomono, aliyekuwa mwenye busara kuliko wafalme wa Israeli, alimaliza hekalu la kwanza, jengo nzuri kuliko ambalo dunia haijaona. Baada ya maangamizi yake kwa Nebukadneza, ikajengwa tena karibu miaka mia tano kabla ya kuzaliwa kwa Kristo.TSHM 3.1

    Lakini hekalu la pili halikulingana na la kwanza katika uzuri. Hakuna wingu la utukufu, hakuna moto kutoka mbinguni, ulioshuka juu ya mazabahu yake. Sanduku, kiti cha rehema, na meza ya ushuhuda havikupatikana pale. Hakuna sauti kutoka mbinguni iliyojulisha kuhani mapenzi ya Mungu. Hekalu la pili halikutukuzwa na wingu la utukufu wa Mungu, lakini lilitukuzwa na kuwako kwa uhai kwa yule ambaye alikuwa Mungu mwenyewe katika mwili. “Mapenzi ya mataifa yote” yalikuja kwa hekalu lake wakati Mtu wa Nazareti alipofundisha na kuponyesha katika viwanja takatifu. Lakini Israeli alikataa zawadi ya matoleo ya mbinguni. Pamoja na Mwalimu mnyenyekevu aliyepita kutoka kwa mlango wake wa zahabu siku ile, utukufu ukatoka hata milele kwa hekalu. Maneno ya Mwokozi yalitimia: “Nyumba yenu imeachwa kwenu tupu”. Matayo 23:38.TSHM 3.2

    Wanafunzi walishangazwa sana kwa utabiri wa Kristo wa maangamizi ya hekalu, na walitamani kufahamu maana ya maneno yake. Herode Mkubwa alitoa kwa ukarimu juu ya hekalu hazina za Waroma na Wayahudi. Vipande vikubwa vya marimari nyeupe, vilipelekwa kutoka Roma, vikafanya sehemu ya ujenzi wake. Kwa mambo haya wanafunzi waliita uangalifu wa Bwana wao, kusema: “Tazama mawe na majengo haya”! Marko 13:1.TSHM 3.3

    Yesu akatoa jibu la wazi na la kushitusha: kweli ninawambia ninyi, Halitabaki jiwe juu ya jiwe pasipo kubomolewa”. Matayo 24:2. Bwana aliwaambia wanafunzi kwamba atakuja mara ya pili. Kwa hiyo, alipotaja hukumu juu ya Yerusalema, mafikara yao yakarejea kwa kurudi, na wakauliza: “Maneno haya yote yatakuwa wakati gani? na nini alama ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia”? Matayo 24:3.TSHM 3.4

    Kristo akaonyesha mbele yao ishara ya mambo makubwa ya kuonekana kabla ya kufungwa kwa wakati. Unabii alioutaja ulikuwa na sehemu mbili maana yake. Wakati ulipokuwa ukitabiri uharibifu wa Yerusalema, unabii huu ulionyesha pia mfano wa matisho ya siku kubwa ya mwisho.TSHM 3.5

    Hukumu zilipashwa kuwekwa juu ya Israeli kwa sababu walikataa na wakasulubisha Masiya. “Basi wakati munapoona chukizo la uharibifu lililosemwa na Danieli nabii, likisimama kwa pahali patakatifu (yeye anayesoma afahamu), halafu wale walio katika Yudea wakimbie kwa milima”. Matayo 24:15,16. Tazama vile vile Luka 21:20,21. Wakati kawaida za kuabudu sanamu za Waroma zitakapo wekwa katika kiwanja kitakatifu inje ya kuta za mji, ndipo wafuasi wa Kristo watapashwa kutafuta usalama katika kukimbia. Wale watakao okoka hawapashwe kuchelewa. Kwa ajili ya zambi zake, hasira ilikwisha kutajwa juu ya Yerusalema. Ugumu wa kuto kuamini kwake ulifanya maangamizo yake ya kweli. Tazama Mika 3:9-11.TSHM 4.1

    Wakaaji wa Yerusalema walimshitaki Kristo kwa chanzo cha taabu zote ambazo zilifika juu yao katika matokeo ya zambi zao. Ingawa walimjua yeye kuwa bila kosa, wakatangaza kifo chake kuwa cha lazima kwa ajili ya salama yao kama taifa. Wakapatana katika maamuzi ya kuhani wao mkuu kwamba inafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu wote, wala taifa lote lisiangamie. Tazama Yoane 11:4753.TSHM 4.2

    Wakati waliua Mwokozi wao kwa sababu alikemea zambi zao, wakajizania wao wenyewe kama watu waliopendelewa na Mungu na kutumainia Bwana kuwakomboa kwa adui zao!TSHM 4.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents