Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  8 / MSHINDI WA UKWELI

  Mfalme mpya, Charles V, akamiliki kwa kiti cha ufalme wa Ujeremani. Mchaguzi wa Saxony ambaye alisaidia Charles kupanda kwa kiti cha ufalme, akamwomba kutotendea Luther kitu chochote mpaka wakati atakapo ruhusu kumusikiliza. Kwa hiyo mfalme akawa katika hali ya mashaka na wasiwasi. Watu wa Papa hawangerizishwa na kitu chochote isipokuwa kifo cha Luther. Mchaguzi akatangaza “Mwalimu Luther anapashwa kutolewa haki (ruhusa ya usalama), ili apate kuonekana mbele ya baraza ya hukumu ya waamzi wenye elimu, watawa, na wa haki wasio na upendeleo.”TSHM 65.1

  Makutano wakakusanyika huko Worms. Kwa mara ya kwanza watoto wa kifalme wa Ujeremani walipashwa kukutana na mfalme wao kijana katika mkusanyiko. Wakuu wa kanisa na wa serkali na mabalozi wa inchi za kigeni wote wakakusanyika kule Worms. Bali jambo ambalo lililoamusha usikivu mwingi lilikuwa la Mtengenezaji. Charles alimuamuru mchaguzi kumleta Luther pamoja naye, kumuhakikishia ulinzi na kuahidi mazungumzo huru juu ya maswali katika mabishano. Luther akamwandikia mchaguzi: “Ikiwa kama mfalme ananiita, siwezi kuwa na mashaka huo ni mwito wa Mungu mwenyewe. Kama wakitaka kutumia nguvu juu yangu, ... Ninaweka jambo hili mikononi mwa Bwana. ... Kama hataniokoa, maisha yangu ni ya maana kidogo. ... Unaweza kutazamia lolote kutoka kwangu ... isipokuwa kukimbia na mimi kukana maneno ya kwanza. Kukimbia siwezi, na tena kukana ni zaidi.”TSHM 65.2

  Kwa namna habari ilienea kwamba Luther alipashwa kuonekana mbele ya baraza, msisimuko ukawa pahali pote. Aleander, mjumbe wa Papa, kwa kujulishwa hatari na akakasirika. Kuchunguza juu ya habari ambayo Papa alikwisha kutolea azabu ya hukumu ingekuwa kuzarau mamlaka ya askofu. Na tena, zaidi mabishano yenye uwezo ya mtu huyu yanaweza kugeuza watoto wa wafalme wengi kutoka kwa Papa. Akamuonya Charles juu ya kutoruhusu Luther kufika Worms na akashawishi mfalme kukubali.TSHM 65.3

  Bila kutulia juu ya ushindi huu, Aleander akaendelea kuhukumu Luther, kushitaki Mtengenezaji juu ya “fitina, uasi, ukosefu wa heshima, na matukano”. Lakini ukali wake ukafunua roho ambayo aliyokuwa ndani yake. “Anasukumwa na fitina na kulipisha kisasi.TSHM 65.4

  Kwa juhudi zaidi tena Aleander akasihi sana mfalme kutimiza amri za Papa. Aliposumbuliwa sana na maombi ya mjumbe Charles akamwomba kuleta kesi yake kwa baraza. Kwa wasiwasi mwingi wale waliopendelea Mtengenezaji wakaendelea kuyatarajia maneno yakasomewa na Aleander. Mchaguzi wa Saxony hakuwa pale, lakini baazi ya washauri wake wakaandika yaliyosemwa na mjumbe wa Papa.TSHM 65.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents