Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  NYONGEZO

  Ukarasa 33 MAJINA YA HESHIMA. Papa Innoncent III alitangaza kwamba mtawa mkuu wa Roma ni “Mwongozi kwa nafasi ya Mungu juu ya dunia, si kama mtu tu, lakini kama Mungu mwenyewe kabisa”. Tazama kitabu kinachoitwa DECRATELS OF THE LORD PAPE GREGORY IX, liber 1, title 7, ch. 3 Corp. Jur. Canon. (2d Leipzig ed. 1881), col. 99.TSHM 332.1

  Juu ya jina la heshima hii ” Bwana Mungu Papa”, tazama maandiko juu ya Extravagantes of Pope John XXII, title 14, Ch. 4, Declaramus. Katika maandiko an Antwerp edition of the Extravagantes, ya mwaka 1584, maneno “Dominum Deum nostrum Papan” (Bwana Mungu wetu Papa) yanaonekana katika kurasa ya 153.TSHM 332.2

  Ukarasa 33. HALI YA KUTOKOSA. Tazama Philip Schaff, The creeds of Christetendom, vol. lI, Dogmatic Decrees of the Vatican Council, pp. 234-271; The Catholic Encyclopedia, vol. VII, art. “Infallibility”; James Cardinal Gibbons, The Faith of Our Fathers (Baltimore : John Murphy Co., 110 th ed., 1917) chs. 7, 11.TSHM 332.3

  Ukarasa 33. IBADA YA SANAMU. “Ibada ya sanamu...ilikuwa moja kati maovu ya Kikristo ambayo yalitambaa ndani ya kanisa kwa siri, karibu bila watu kuchunguza.ao kutambua.. Kidogo kidogo, desturi ikafuata ingine kutokana na ibada hiyo, na kanisa ikaanguka ndani ya ibada ya sanamu, ... karibu bila kukemewa; na wakati walijaribu kufanya juhudi ya kuingoa, uovu ulionekana kuwa mwenye kuzidi sana na hauwezi kuondolewa J. Mendham, The General Council, the Second of Nicaea, Utangulizi, pp. iii-vi.TSHM 332.4

  Juu ya habari ya mazungumuzo na mipango ya Baraza ya Nicaea, mwaka 787 A.D ilikusanyika kwa kusimamisha ibada ya sanamu, tazama maandiko A Select Library of Nicene and PostNicene Fathers, second series, vol XIV, pp 521-587 (New York, 1900); C.J. Hefele, A History of the Councils of the Churches, From the Original Documents, bk. 18, Ch. 1, secs. 332,333; Ch. 2, Secs. 345352 (T. and T. Clark, ed. 1896), vol. 5, pp. 260-304, 342-372.TSHM 332.5

  Ukarasa 34. SHERIA YA SIKU YA KWANZA YA CONSTANTI-NO, sheria hii imetolewa katika Kilatini na katika fasiri ya Kiingereza ndani ya kitabu kinachoitwa Philip Schaff’s “History of the Christian Church” (historia ya kanisa la Kikristo) kilichoandikwa na Philip Schaff, vol III, 3 d period, Ch. 7, sec 75, p.38o, foot note 1. Tazama mazungumuzo katika kitabu cha Albert Henry Newman, A Manual of Church History (Philadelphia: The American Baptist Publication Society, 1933), rev. ed., vol. I, PP. 305-307; na katika kitabu cha L. E. From, The Prophetic Faith of Our Fathers (Washington, D.C.: Review and Herald Publishing Assn, 1950), vol. I, pp. 376-381.TSHM 332.6

  Ukarasa 35. TAREHE ZA UNABII. Kanuni ya muhimu katika maelezo ya nyakati za unabii ni kanuni ya siku-mwaka-ambayo inakamata siku moja ya wakati wa unabii kama mwaka mumoja wa kalendari ya wakati. Sababu fulani fulani za Biblia juu ya kanuni hii ni kama zifuatazo : (1) kanuni ya siku-mwaka inapatana na kanuni ya kueleza mifano ya nyama kama falme, pembe kama uwezo, bahari kama watu, na kazalika. (2) Bwana, anaposema katika Hesabu 14:34 na katika Ezekieli 4:6 anaunga mukono kanuni hii. (3) siku 2300 (miaka) ya Danieli 8:14 inafunika historia ya falme za wa Medi na Wapersia, wa Giriki na Waroma, kama vile malaika anavyoeleza katika mistari 19-26 ( kwa wakati wa mwisho maono haya yatatimia ). Falme hizi zilidumu kwa nyakati ndefu zaidi ya siku za kawaida 2300. Hakuna lolote litakalo stahili isipokuwa kanuni ya siku-mwaka (4) Danieli 11 ni upanuo wa unabii wa Danieli 8, lakini Danieli 11 si unabii wa mufano. Mara tatu unabii huu unasema juu ya “miaka” (mistari 6, 8, 13) sawasawa na “siku” katika Danieli 8:14. (6) Malaika alielezea Danieli kwamba unabii haya yanaelekea “wakati wa mwisho” (8:19, 26; 10:13, 14). Kama “siku” zingekuwa na namna ilivyo wazi, unabii a haungekuwa na maana.(7) Siku moja kama mwaka ilikuwa kawaida ya kusema katika kiebrania cha Agano la Kale. Tazama Walawi 25:8; Mwanzo 29:27. (8) Kitabu cha Ufunuo kinafungua unabii wa Danieli, kikionyesha kwamba kutimilika kwazo ni kwa wakati ujao wakati wa mitume. Zaidi ya hayo, kanuni ya siku _ mwaka ilitambuliwa na kukubaliwa wanafunzi waangalifu wa Biblia kama kanuni yenye sheria. Wamoja waa wanafunzi hawa kunakuwa Joachim wa Floris, Wychiffe, Joseph Mede, bwana Isaac Newton, Askofu Thomas Newton, Alexander Keith na wengine wengi.TSHM 333.1

  Ukarasa 37. MAANDIKO YA UWONGO. Miongoni mwa maandiko yaliyokubaliwa kwa kawaida kuwa ya uwongo: Donation of Constantine na Pseudo-Isidorian Decretals inakuwa ya muhimu sana. Tazama maandiko The New Schaff-Herzog Encyclopedia of Religious Knowledge, vol.III. “Donation of Constantine” (Zawadi ya Constantino).TSHM 333.2

  Maandiko hii “Pseudo-Isidorian Decreals” ilikuwa mabarua ya uwongo yalioandikwa kwa wa Papa wa kwanza kutoka Clementino (mwaka 100 A.D nyuma ya Kristo) hata Papa Gregoire Mkuu (mwaka 600 A.D nyuma ya Kristo) na baadaye yalichanganywa na mkusanyo wa maandiko ya karne ya tisa kusudi wanazania kwamba yaliandikwa na “Isidore Mercator”. Udanganyifu wa “Pseudo-lsidorian” kufanyizwa kama jengo kunakubaliwa sasa.TSHM 334.1

  Ukarasa wa 38. TOHARANI . Dr Joseph Faa Di Bruno anaeleza hivi toharani: “Toharani, ni hali ya mateso baada ya maisha haya, ambayo zile roho zinafungwa kwa muda, zile ambazo huaga maisha aya baada ya kusamehewa zambi za mauti kama kwa alama na kosa, na kama kwa mateso ya milele ambayo yalisababishwa nao, lakini ambao wangali na deni ya kulipa kwa mateso ya fulani, kama vile vile roho zile ambazo zinaaga dunia zikiwa na makosa ya zambi ndogo ndogo tu-Catholic Belief, p. 196 (ed. 1884; imprimatur Archbishop of New York). Tazama The Catholic encyclopedia, vol.XII, art. “Purgatory”.TSHM 334.2

  Ukarasa 39. UNUNUZI WA MUSAMAHA (indulgences). Kwa historia kamili ya kila kitu ya mafundisho juu ununuzi wa musamaha, tazama mafundisho The Catholic Encyclopedia art. “Indulgences”, vol VII; A.H Newrman, A Mannual of Church History (Kanuni ya Historia ya kanisa) Philadelphia: The American Baptist Publication Society, 1953 vol. II, pp. 53,54,62.TSHM 334.3

  Ukarasa 44. SABATO KATIKATI YA WAFUASI WA WALDENSE Kunakuwa ushahidi unao kuwako juu ya kushika sabato ya siku ya saba miongoni mwa Waldense. Habari moja juu ya mahakama ya Papa ambayo mbele yake kulipelekwa wafuasi fulani wa Waldense wa Marovia katikati ya karne ya kumi na tano, inatangaza kwamba miongoni mwa Waldense “wengi walitukuza Sabato ya Wayuda”. Johann Joseph Ignaz Von Dollinger, Beitrage Zur Sektengeschichte des Mittelalters (Contributions to the Historya of the Sects of the Middle Ages), Munich, 1890, part 2, p. 661.TSHM 334.4

  Ukarasa 49. AMRI JUU YA WAFUASI WA WALDENSE. Kipande cha barua ya Papa (Innocent VIII, 1487) kupinga wa Waldense kimetolewa katika fasiri ya kiingereza, ndani ya maandiko Dowling’s History of Ramanism, bk. 6, ch. 5, sec. 62 (ed. 1871).TSHM 334.5

  Ukarasa 53. UNUNUZI WA MUSAMAHA. Tazama nukta kwa p. 39.TSHM 335.1

  Ukarasa 53, 60. WYCLIFFE. Kwa mandiko ya asili ya barua za Papa za kupinga Wycliffe pamoja na tafsiri ya Biblia katika kiingereza, tazama Jonn Foxe, Acts and Monuments of the Church (London: Pratt Townsend, 1870) vol. Ill, pp. 4-13; Merle d’aubigné, The History of the Reformation in the sixteenth Century (historia ya Matengenezo katika karne ya kumi na sita) (London): Blackie and Son, 1885), vol. IV, div. 7. p. 93; Philip Schaff, History of the Christian Church (New York: Chas. Scribner’s Sons, 1915), vol. V Part 2, p. 317.TSHM 335.2

  Ukarasa 54. HALI YA KUTOKUKOSA Tazama nukta kwa p.33.TSHM 335.3

  Ukarasa 64. UNUNUZI WA MUSAMAHA Tazama nukta p. 39.TSHM 335.4

  Ukarasa 64. BARAZA LA CONSTANCE. Vitabu vya siku hizi juu ya Baraza hii ni: K. Zähringer, Das Kardinal Kollegium auf dem Konstanzer Konzil (Munster, 1935); Th. F. Grogau, The Conciliar Theory as it Manifested Itself at the Council of Constance (Washington, 1949); Fred A Kremple, Cultural Aspects of the Council of Constance and Basel (Ann Arbor, 1955).TSHM 335.5

  Tazama John Huss, Letters (barua), 1904; E.J. Kitts, Pape John XXIII and Master John Huss (London, 1910); D. A. Schaff, John Huss (1915); na Matthew Spinka, John Huss and the Czech Reform (1941).TSHM 335.6

  Ukarasa 81. UNUNUZI WA MUSAMAHA Tazama nukta kwa p.39TSHM 335.7

  Ukarasa 146. MWENENDO WA WASHIRIKI WA JAMII LA YESU (JESUITISM). Kuhusu washiriki wa Jamii la Yesu, tazama kitabu Concerning Jesuits, kilitayarishwa na Rev. John Gerard, S.J. (London: otholic Truth Society, 1902). Katika kazi hii, wanasema kwamba “msingi maalumu wa utaratibu wote wa Jamii ni roho ya utii kamili: “Acha kila mtu”, anaandika St. Ignatius, “mashawishwa mwenyewe kwamba wale wanaoishi chini ya utii wanapashwa kujiruhusu wao wenyewe kuendeshwa na kuongozwa na maagizo ya Mungu kupitia wakubwa wao, sawa kama vile wangekuwa maiti, ambayo inajiruhusu kupelekwa mahali popote na kutendewa hali yoyote ao kama vile fimbo (gongo) la mzee analolitumia kulishika mkononi kwa namna yote anayoweza” p.6.TSHM 335.8

  Ukarasa 147. MAHAKAMA YA PAPA. Tazama kitabu The Catholic Encyclopedia, vol. VIII, art. “Inquisition”; na E. Vacandard, The Inquisition: A Critical and Historical Study of the Coercive Power of the Church (New York: Longmans, Green, and Company, 1908).TSHM 336.1

  Kuhusu maoni ya watu ambao si wakatoliki, tazama Philip Van Limborch, History of the Inquisition; Henry C. Lea, A History of the Inquisition in the Middle Ages, 3 vols. TSHM 336.2

  Ukarasa 166. SABABU ZA MAPINDUZI YA UFARANSA. Tazama H. Von Sybel, History of the French Revolution, bk.5, ch. 1, pars. 3-7; H. T. Buckle, History of Civilization in England, chs. 8, 12, 14 (New York, ed. 1895), voI.I, pp.364-366, 369-371, 437, 540, 541, 550; Blackwood’s Magazine, vol. XXXIV, no 215 (November, 1833), p. 739; J.G. Lorimer, An Historical Sketch of the Protestant Church in France, ch. 8, pars. 6, 7.TSHM 336.3

  Ukarasa 167. TAREHE ZA UNABII Tazama nukta kwa p. 35.TSHM 336.4

  Ukarasa 167. JUHUDI ZA KUFUTA NA KUANGAMIZA BIBLIA. Baraza la Toulouse liliamuru: “Tunakataza watu wasioviongozi wa dini kuwa na maandiko ya Agano la Kale na agano Jipya...Tunawakataza vikali sana zaidi kuwa na vitabu hivi katika lugha ya kusemwa na wakaaji wote”. ” Makao, nyumba nyenyekevu sana za wamaskini, na hata maficho ya chini chini ya wale watu wanaosadiki kuwa na Maandiko yataangamizwa. Watu hawa watawindwa ndani ya pori na pango na mtu ye yote atakayewapatia ulinzi atahukumiwa vikali”. Council Tolosanum, Gregory IX, (Papa Gregori wa IX) Anno chr. 1229. Canons 14, 2. Baraza hili lilikaa lilifanyika wakati wa vita ya Papa kupinga watu wa Albi (kwa kifaran-sa albigeois).TSHM 336.5

  “Tauni hili (Biblia) ilikuwa imekwisha kufikia eneo kubwa kwa namna watu fulani walikuwa wamejichagu lia mapadri wao wenye-we, na hata wahubiri fulani ambao waligeuza na kuharibu ukweli wa habari njema na kufanya habari njema mpya juu ya makusudi yao wenyewe... (wanajua kwamba) mahubiri na maelezo ya Biblia inakatazwa kwa washiriki”. Acts of Inquisition, Philip Yan Limborch, History of the Inquisition, ch. 8.TSHM 336.6

  Kwa Baraza la constance kwa mwaka 1415, Wycliffe alihukumiwa akisha kufa kama “yule maskini wa kunuka tauni ya uzushi wa kulaaniwa ambaye alivumbua tafsiri mpya ya Maandiko katika lugha yake ya asili”.TSHM 336.7

  Upinzani kwa Biblia wa kanisa la Kikatoliki la Roma uliongezeka kwa sababu ya usitawi wa vyama vya Biblia. Kwa tarehe 8, mwezi wa 12, mwaka 1866, Papa Pius IX, katika barua yake kwa Maaskofu wote, inayoitwa Quanta Cura, alitoa hesabu ya makosa munane na kuelezwa chini ya vipindi kumi mbalimbali. Chini ya kipindi IV tunapata orosa ya: “Ujamaa, Ukomunisti, vyama vya kisirisiri, vyama vya Biblia... Tauni za aina hii zinapashwa kuangamizwa kwa njia zote ziwezekanavyo”. Katika miaka ya karibu kulitokea mabadiliko ya kushangaza na ya hakika katika kanisa la Kikatoliki la Roma. Kwa upande moja kanisa limekubali tafsiri nyingi zilizotayarishwa kufuatana na lugha ya asili ya Biblia; kwa upande mwingine liliendelesha kujifunza kwa Maandiko matakatifu kwa njia ya kugawia watu bure na kwa njia ya mashirika ya Biblia. Kanisa, lakini, linaendelea kujiwekea haki ya pekee ya kueleza Biblia kufuatana na nuru na desturi yake mwenyewe, ili kutibitisha yale mafundisho ambayo hayaambatane na mafundisho ya Biblia.TSHM 337.1

  Ukarasa 173. UTAWALA WA KUTISHA Kwa utangulizi aminifu kwa historia ya Mapinduzi ya Ufaransa, tazama L. Gershoy, The French Revolution (1932). G.Lefebvre, The Coming of the French Revolution (kuja kwa mapinduzi ya Ufransa) (Princeton. 1947); na H. Von Sybel, History of The French Revolution, 4 vols. (1869). Angalia na A. Aulard, Christianity and the French Revolution (London, 1927), ambacho ndaniyake historia inaendelea hata 1802 ni majifunzo bora.TSHM 337.2

  Ukarasa 175. WATU WENGI WA HALI YA CHINI NA WAHESHIMIWA WA HALI YA JUU Angalia H. Von Holst, Lowell Lectures on French Revolution, lecture 1; tena angalia Taine, Ancient Regime; na A Young, Travels in France.TSHM 337.3

  Ukarasa 177. MALIPIZI. Angalia Thos. H. Gill, The Papal Drama, bk. 10 E. de Presensé, The Church and The French Revolution, (kanisa na mapinduzi ya Ufransa) bk. 3, ch. 1.TSHM 337.4

  Ukarasa 177. UKATILI WA UTAWALA WA KUTISHA. Angalia M.A. Thiers, History of rhe French Revolution (New York, ed. 1890, tr. by F. Shobert), vol. 3, pp. 42-44, 62-74, 106; F.A. Mignet, History of the French Revolution (Bohn, ed. 1894), ch. 9, par. 1; Sir Archibald Alison, History of Europe, From the Commencement of the French Revolution to the Restoration of Bourbons, vol.l, ch. 14 (New York, ed. 1872), vol. 1, pp. 293-312.TSHM 337.5

  Ukarasa 179. MUZUNGUKO WA MAANDIKO. Kwa mwaka 1804, kutokana na Mr William Canton, wa shirika la Biblia linaloitwa “British and Foreign Bible Society”, Biblia zote zinazokuwa ulimwenguni, zilizoandikwa kwa mikono ao kwa machini, ukihesabu kila tafsiri katika kila inchi, kwa kuhesabiwa hazikuwa zaidi ya milioni ine.TSHM 338.1

  Tangu 1816 1981, Shirika la Biblia la Amerika peke yake lilichapisha nakala (copies) 98.200.951 za Biblia yote nzima na nakala za hesabu za Biblia 3.396.127.592. Kwa mwaka 1981, Shirika la Biblia la Amerika lilichapisha nakala za Biblia yote nzima 3.365.779. Shirika za Biblia zingine ziliongeza mamilioni mengi za nakala kwa hesabu hizi.TSHM 338.2

  Ukarasa 179. UJUMBE KWA INCHI YA KIGENI Kazi ya kuhubiri injili ya kanisa la kristo la mwanzo ilikuwa kwa kweli imekufa kwa mwaka 1000, na ilifuatwa na mashambulio ya vita za Papa. Wakati wa Matengenezo kazi ya kuhubiri injili katika ugenini ilionekana kuwa hafifu. Uamsha wa utawa ulizaa waeenezaji wa injili. Kazi la kanisa ya la Moravi kwa karne la kumi na munane ilikuwa ya kuonekana sana, na kulipatikana shirika fulani za waenezaji wa injili ambazo zilizofanywa na Uingereza kwa ajili ya kazi katika inchi za kikoloni ya Amerika ya kaskazini. Lakini jambo muhimu zaidi la kazi ya uenezaji wa injili ulioanza karibu mwawka 1800, kwa “wakati wa mwisho” (Dan. 12-4). Katika mwaka 1792, Shirika la Uenezaji wa injili la Wabatista lilituma Carey kwa inchi ya India. Kwa mwaka wa 1795, Shirika la London Missionary lilitengenezwa na shirika lingine kwa mwaka 1799, ambalo kwa mwaka 1812 liligeuka kuwa shirika linaloitwa Church Missionary Society. Nyuma kidogo Shirika la Uenezaji wa Injili la WaMetodisti wa Wesley (Wesleyan Methodist Society) likaafanya. Katika mwaka 1812 Muungano wa inchi za Amerika ulianzisha shirika linaloitwa American Board of Commissioners for Foreign Missions (Baraza la Amerika la Wajumbe kwa inchi za kigeni na kwa mwaka ule Adoniran Judson akatumwa huko Calcutta. Mwaka uliofuata akaweka makao yake pale Burma. Kwa mwaka 1814 kulianzishwa Muungano wa Uenezaji wa Injili wa Wabatista wa Amerika. Kwa mwaka 1837 kulianzishwa Baraza linaloitwa Presbyterian Board of Foreign Missions.TSHM 338.3

  “Kwa mwaka 1800 nyuma ya Yesu, wingi wa Wakristo wa nguvu walikuwa vizazi vya wale ambao wamageuka mbele ya mwaka 1500 nyuma ya Kristo... Sasa kwa karne ya kumi na tisa, dini ya Kristo iliongezeka... Hakuna wakati wa maendeleo ule ambao kanisa la Kikristo liliinuka kwa mashirika kwa wingi wa namna hii. Hakuna wakati kanisa la kikristo liliikuwa na mguso wa moyo wa watu wa Ulaya ya Mangaribi. Juhudi nyingi hizi ndizo zilileta kazi ya kuanzisha shirika ya Uenezaji wa Injili, ambayo kwa karne ya kumi na tisa iliongeza watu na mvuto wa Kikristo”. Kenneth Scott Latourette, A History of the Exppansion of Christianity, vol. IV, The Great Century, A.D 1800 A.D. 1914 (New Yorks: Harper and Bross., 1914), pp. 2-4. TSHM 339.1

  Ukarasa 203. SIKU MOJA KWA MWAKA MMOJA Angalia nukta kwa p.35.TSHM 339.2

  Ukarasa 205. MWAKA 457 MBELE YA YESU. Kwa uhaki wa tarehe ya mwaka 457 mbele ya Yesu kwamba ni mwaka wa saba wa utawala wa mfalme Artasasta, angalia S.H. Horn na L.H. Wood, The Chronology of Ezra 7 (Washington, D.C.: Review and Herald Publishing Association, 1953); E.G. Kraeing, The Brooklyn Museum Aramaic Papyri (New Haven or London, 1953), pp. 191-193; “The Seventh -day Adventist Bible Commentary” (Washington, D.C.: Review and Herald Publishing Association, 1954), vol. Ill, pp. 97-110.TSHM 339.3

  Ukarasa 209. KUANGUKA KWA UFALME WA UTURKIA Katika wakati wote wa Matengenezo, Uturkia ulikuwa unaleta woga kila wakati kwa Ulaya ya Kikristo; maandiko ya Watangenazaji yanajaa na hukumu juu ya utawala wa Uturkia. Tangu wakati huu waandishi wa Kikristo walihusika na daraka la Uturkia katika tukio ya wakati ujao, na waandishi wa maelezo juu ya unabii wameona uwezo wa Uturkia na kuanguka kwake kulikotangazwa na Maandiko mbele ya wakati.TSHM 339.4

  Kwa unabii wa “sasa, siku, mwezi, mwaka”, kama sehemu ya baragumu la sita, Josiah Litch alionyesha matumizi ya wakati wa unabii, wa kumaliza Uhuru wa Uturkia kwa mwezi wa munane, mwaka 1840.TSHM 339.5

  Kitabu cha Uriah Smith kinachoitwa Thoughts on Daniel and the Revelation (Mawazo juu ya Danieli na Ufunuo), rev.ed.of 1944, kinazungumza juu ya hesabu ya wakati wa utabiri huu kwa namna ya unabii kwa karasa za 506-517.TSHM 339.6

  Ukarasa 232. KANZU ZA MUPANDO. Hadizi ambayo inasema kwamba Waadventist walitengeneza kanzo ambazo watapanda nazo “kumulaki Bwana hewani” ilitungwa na wale ambao walitamani kulaumu mahubiri kuhusu kurudi kwa Yesu. Uchunguzi wa uangalifu ulionyesha uwongo kwa hadizi hii.TSHM 340.1

  Maandiko ya kanusha hadizi hii ya kanzu za kukaa kwa kupanda mbinguni, tazama Francis D.Nichol, The midnight Cry (Washington, D.C.: Review and Herald Publushing Association, 1944), chs.25-27, and Appendices H.J.tazama pia LeRoye From, The Prophetic Faith of Fathers (Washington, D.C.: Review and Herald Publishing Association, 1954), vol. IV, pp 822-826.TSHM 340.2

  Ukarasa 269. UJUMBE MARA TATU. Ufunuo 14-6,7 inasema mbele ya wakati juu ya utangazaji wa ujumbe wa malaika wa kwanza. Kwa hivyo nabii anaendelea: “Malaika mwingine akamfuata akisema: Umeanguka, umeanguka, Babeli,... na malaika wa tatu akawafuata. Neno lililotafsiriwa hapa “akafuata” maana yake ni “kwenda pamoja na”, “kufuata mmoja”, “kwenda naye”. Tena maana yake ni “kusindikiza”. Wazo walitaka kutoa ni la “kwenda pamoja”, “kuwa pamoja”. Wazo la Ufunuo 14:8,9 si kwamba malaika wa pili na wa tatu walifuata tu malaika wa kwanza katika hatua ya wakati, lakini wazo ni kwamba walienda pamoja naye. Ni watatu tu kwa utaratibu wa kutokea kwao. Lakini wakisha tokea, wanaendelea pamoja.TSHM 340.3

  Ukarasa 352. CHEO CHA UWEZO WA MASKOFU WA ROMA. Angalia kitabu cha James Cardinal Gibbons, Faith of Our Fathers (Baltimore: John Murphy Co., 110th ed., 1917), chs. 5,9,10,12.TSHM 340.4

  Ukarasa 352. SABATO MIONGONI MWA WALDENSE. Angalia nukta kwa p. 44.TSHM 340.5

  Ukarasa 353. KANISA LA ETIOPIA NA SABATO. Kanisa la Etiopia linaloitwa Kopta (Coptic) lilishika Sabato ya siku ya saba mpaka hapo majuzijuzi. Waetiopia vile vile walishika siku ya Kwanza (dimanche). Uchungaji wa Sabato ya siku ya saba, kwa kweli karibu kumesimama katika Etiopia ya sasa. Kuhusu maelezo ya washahidi waliojionea kwa macho mambo ya siku za dini katika Etiopia, angalia Pero Gomes de Teixeira, The Discovery of Abissinia by the Portuguese in 1520 (kilichotafsiriwa kwa kingereza huko London: British Museum, 1938), p.79; Father Francisco Alvarez, Narrative of the Portuguese Embassy to Abyssinia During the Years 1520-1527, in the Records of the Hakluyt Society (London, 1881), vol. LXIV, pp. 22-49.TSHM 340.6

  Maneno yengine na vitabu vilivyotagiwa waweza kuyachunguza katika kitabu kama hiki kwa lugha ya Kingereza: From Here to Forever.TSHM 341.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents