Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Utawala wa Hofu Kuu

    Mfuasi maskini wa imani ya matengenezo aliyezoea kuita waaminifu kwa mikutano ya siri akakamatwa. Kwa kutishwa juu ya kifo cha gafula kwa mti wa kuchomwa, akaamuriwa kuongoza mjumbe wa Papa kwa nyumba ya kila mprotestanti katika mji. Hofu ya ndimi ya moto ikawa nyingi sana, na akakubali kusaliti ndugu zake. Morin, polisi wa mfalme, pamoja na msaliti, kwa polepole na ukimya akapita katika njia za mji. Walipofika mbele ya nyumba ya mtu mmoja wa Luther, msaliti akafanya ishara, lakini bila kusema neno. Mwandamano ukasimama, wakaingia nyumbani, jamaa likakokotwa na kufungwa minyororo, na mfuatano wa kutisha ukaendelea katika kutafuta watu wengine wapya wa kutesa. “Morin akatetemesha mji wote. ... Ulikuwa utawala wa hofu kuu.”TSHM 103.4

    Watu walioteswa wakauawa kwa mateso makali, ikaamriwa kwamba moto upunguzwe ili kuzidisha mateso yao. Lakini walikufa kama washindaji, musimamo wao usiotikisika, amani yao kamili. Watesi wao wakajiona wenyewe kwamba walishindwa. “Watu wa Paris wote wakapata nafasi ya kuona aina gani ya watu mawazo mapya yaliweza kuleta. Hakuna mimbara ilikuwako kwa kulinganishwa na mjumba kubwa la wafia dini. Furaha ikaangazia nyuso kunjufu za watu hawa wakati walipokuwa wakielekea ... pahali pa kuuawa ... na kuomba kwa usemaji wa kushangaza kwa ajili ya injili.”TSHM 104.1

    Waprotestanti wakasitakiwa kwamba walikusudia kuua wakatoliki, kupindua serkali, na kumua mfalme. Hawakuweza kutoa hata kivuli cha ushahidi kwa kushuhudia mambo yenyewe. Huku ukali ukapiga juu ya Waprotestanti wasio na kosa ukaongezeka kwa uzito wa malipizi, na katika karne zilizofuata kukatokea maangamizi ya namna ile waliyotabiri juu ya mfalme, serkali yake, na raia wake. Lakini yakaletwa na wakafiri na wakatoliki wao wenyewe.TSHM 104.2

    Kuvunja dini ya Kiprotestanti ndiko kulileta juu ya Ufransa misiba hii ya kutisha. Mashaka, hofu, na vitisho sasa vikaenea kwa makundi yote ya jamii. Mamia wakakimbia kutoka Paris, wakajihamisha wenyewe kutoka inchini mwao ya kuzaliwa, wengi kati yao wakatoa ishara ya kwanza kwamba walikubali imani ya matengenezo. Wafuasi wa Papa wakashangazwa na hesabu kubwa ya “wapinga ibada ya dini” isiyofikiriwa iliyovumiliwa miongoni mwao.TSHM 104.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents