Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Zwingli Akaitwa Zurich

  Baada ya miaka mitatu Zwingli akaitwa kuhubiri katika kanisa kubwa la Zurich, mji mkubwa sana wa ushirika wa Suisi. Mvuto uliotumiwa hapa ulisikuwa mahali pengi. Wapadri waliomwita kwa kazi hiyo wakawa na uangalifu wa kumfahamisha hawakutaka mageuzi:TSHM 81.1

  “Utaweka juhudi yote kukusanya mapato kwa mfululizo bila kusahau kitu cho chote. ... Utakuwa na juhudi ya kuongeza mapato kutoka kwa wagonjwa, kwa misa, na kwa kawaida kutoka kwa kila agizo la dini.” “Juu ya uongozi wa sakramenti, mahubiri, na ulinzi wa kundi, ... unaweza kutumia mtu mwingine, na zaidi sana katika mahubiri.”TSHM 81.2

  Zwingli akasikiliza kwa ukimya kwa agizo hili, na akasema kwa kujibu, “Maisha ya Kristo yamefichwa mda mrefu kwa watu. Nitahubiri juu habari yote ya Injili ya Mtakatifu Matayo. ... Ni kwa utukufu wa Mungu, kwa sifa ya mwana wake, kwa wokovu wa kweli wa roho, na kwa kujijenga katika imani ya kweli, ambapo nitajitoa wakfu kwa kazi yangu.”TSHM 81.3

  Watu wakajikusanya kwa hesabu kubwa kwa kusikia mahubiri yake. Akaanza kazi yake kwa kufungua Injili na kueleza maisha, mafundisho, na mauti ya Kristo. “Ni kwa Kristo,” akasema, “ambapo natamani kuwaongoza ninyi--kwa Kristo, chemchemi ya kweli ya wokovu.” Wenye maarifa ya utawala, wanafunzi, wafundi, na wakulima wakasikiliza maneno yake. Akakemea makosa bila hofu na maovu ya nyakati. Wengi wakarudi kutoka kwa kanisa kuu wakimusifu Mungu. “Mtu huyu,” wakasema, “ni mhubiri wa ukweli. Atakuwa Musa wetu, kutuongoza kutoka katika giza hii ya Misri.”TSHM 81.4

  Baada ya wakati upinzani ukaanza. Watawa wakamushambulia kwa zarau na matusi; wengine wakatumia ukali na matisho. Lakini Zwingli akachukua yote kwa uvumilivu.TSHM 81.5

  Wakati Mungu anapojitayarisha kuvunja viungo vya pingu vya ujinga na ibada ya sanamu Shetani anatumika na uwezo mkubwa sana kwa kufunika watu katika giza na kufunga minyororo yao kwa nguvu zaidi. Roma ikaendelea kutia nguvu mpya kwa kufungua soko yake katika mahali pote pa Ukristo, ukitoa msamaha kwa mali. Kila zambi ilikuwa na bei yake, na watu walipewa chetibila malipo kwa ajili ya zambi kama hazina ya kanisa ililindwa yenyekujaa vizuri. ... Hivi mashauri mawili haya yakaendelea--Roma kuruhusu zambi na kuifanya kuwa chemchemi ya mapato yake, Watengenezaji kulaumu zambi na kuonyesha Kristo kama kipatanisho na mkombozi.TSHM 81.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents