Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  “Kilio cha Usiku wa Manane”

  Maneno yakawa na hakikisho la nguvu, na “kilio cha usiku wa manane” kikasikiwa kwa maelfu ya waaminifu. Kama mawimbi, tukio hili likazambaa kwa nguvu toka mji kwa mji, kijiji kwa kijiji. Ushupavu ukatoweka kama baridi kali ya alfajiri kabla ya jua kutokea. Kazi ilikuwa ya namna moja na ile ya nyakati za kurudi kwa Bwana ambako miongoni mwa Israeli wa zamani walifuata ujumbe wa karipio kutoka kwa watumishi wake. Hapo kulikuwa furaha nyingi sana, lakini Zaidi uchunguzi mwingi wa moyo, ungamo la zambi, na kuacha dunia. Hapo kulikuwa kujitoa wakfu kwa Mungu.TSHM 191.4

  Kwa miendo yote ya dini tangu siku za mitume, hakuna mojawapo yaliojiepusha zaidi kwa upungufu wa kibinadamu na werevu wa Shetani kuliko ile iliokuwa kwa wakati wa masika ya mwaka 1844.TSHM 192.1

  Kwa mwito, “Tazama bwana arusi anakuja,” wale waliokuwa wakingojea “wakaamka, wakatengeneza taa zao”; wakajifunza Neno la Mungu kwa usikizi mkuu ambao haukuwako mbele. Hawakukuwa wenye vipawa zaidi, bali wenye kuwa wenye unyenyekevu zaidi na wenye bidii, waliokuwa wa kwanza kutii mwito. Wakulima wakaacha mavuno yao katika mashamba, wafundi wa mashine wakaacha vyombo vyao na kwa furaha wakaenda kutoa maonyo. Makanisa kwa kawaida yakafunga milango yao juu ya ujumbe huu, na kundi kubwa la wale walioukubali wakajitenga kwao. Wasiosadiki waliokusanyika kwa mikutano ya Waadventiste wakaona uwezo wa kusadikisha ukihuzuria ujumbe, “Tazama, bwana arusi anakuja!” Imani ikaleta majibu kwa maombi. Kama manyunyu ya mvua juu ya inchi yenye kiu, Roho ya neema akashuka juu ya watafutao kwa bidii. Wale waliotazamia upesi kusimama uso kwa uso pamoja na Mkombozi wao wakaona furaha kubwa. Roho Mtakatifu akalainisha moyo.TSHM 192.2

  Wale waliokubali ujumbe wakafikia wakati ambao walitumainia kukutana na Bwana wao. Wakaomba sana mtu kwa mwenzake. Wakakutana mara kwa mara katika mahali pa uficho kushirikiana pamoja na Mungu, na sauti ya maombezi ikapanda mbinguni kutoka mashambani na vichakani. Hakikisho la kibali cha Mwokozi yalikuwa ya lazima zaidi kwao kuliko chakula cha kila siku, na kama wingu lilitia giza katika akili zao, hawakutulia hata walipoona ushuhuda wa neema ya rehema.TSHM 192.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents