Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  10 / MAENDELEO KATIKA UJEREMANI

  Kutoweka kwa ajabu kwa Luther kukaweka Ujeremani wote katika hofu kubwa. Habari ikatangazwa na wengi wakaamini kwamba aliuawa. Kukawa maombolezo makubwa, na wengi wakaapa kwa kitisho kulipiza kisasi cha kifo chake.TSHM 85.1

  Ijapo waiishangilia mara ya kwanza kwa ajili ya kifo kilichozaniwa cha Luther, adui zake walijazwa na hofu kuwa sasa kwamba amekuwa mfungwa. “Njia moja tu inayotubakilia kwa kuokoa kesi letu,” akasema mmoja wao, “ni kuwasha mienge, na kumuwinda Luther katika ulimwengu wote na kumrudisha kwa taifa linalomwita.” Kusikia kwamba Luther alikuwa salama, ijapo alikuwa mfungwa, jambo hili likatuliza watu, huku wakisoma maandiko yake kwa bidii sana kuliko mbele. Hesabu ya wale walioongezeka wakajiunga kwa kisa cha mshujaa aliyetetea Neno la Mungu.TSHM 85.2

  Mbegu ambayo Luther alipanda ikatoa matunda mahali pote. kutokuwapo kwake kukafanya kazi ambayo kuwako kwake hakungeweza kufanya. Na sasa mwongozi wao mkuu ameondolewa, watumikaji wengine wakafanya bidii ili kazi ya maana sana iliyoanzishwa isipingwe.TSHM 85.3

  Sasa Shetani akajaribu kudanganya na kuangamiza watu kwa kuwapokeza kazi iliyogeuzwa kwa hila pahali pa kazi ya kweli. Kwa namna kulikuwa Wakristo wa uongo kwa karne la kwanza, ndipo kukatokea manabii wa uongo kwa karne ya kumi na sita.TSHM 85.4

  Watu wachache wakajizania wenyewe kupokea mafumbulio ya kipekee kutoka Mbinguni na kuchaguliwa na Mungu kwa kutimiza kazi ya Matengenezo ambayo ilianzishwa kwa uzaifu na Luther. Kwa kweli, walibomoa kile Mtengenezaji alichofanya. Walikataa kanuni ya Matengenezo kwamba Neno la Mungu ni amri moja tu, ya kutosha ya imani na maisha. Kwa kiongozi kile kisichokosa wakaweka maagizo yao yasiyokuwa ya hakika, ya mawazo yao wenyewe na maono.TSHM 85.5

  Wengine kwa urahisi wakaelekea kwa ushupavu na kujiunga pamoja nao. Mambo ya wenye bidii hawa yakaleta mwamsho mkubwa. Luther alikuwa ameamsha watu kuona haja ya Matengenezo, na sasa watu wengine waaminifu wa kweli wakaongozwa vibaya na madai ya “manabii” wapya.TSHM 85.6

  Waongozi wa kazi wakaendelea pale Wittenberg na wakalazimisha madai yao juu ya Melanchton: “Tumetumwa na Mungu kwa kufundisha watu. Tulikuwa na mazungumzo ya kawaida pamoja na Mungu; tunajua jambo litakalotokea; kwa neno moja, tunakuwa mitume na manabii, na tunatoa mwito kwa Mwalimu Luther.”TSHM 85.7

  Watengenezaji wakafazaika. Akasema Melanchton; hapa panakuwa kweli roho za ajabu katika watu hawa; lakini roho gani? ... Kwa upande mwengine tujihazari kuzima Roho wa Mungu, na kwa upande mwengine, kwa kudanganywa na roho ya Shetani.”TSHM 86.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents