Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  11 / USHUHUDA WA WAANA WA WAFALME

  Mojawapo ya shuhuda “maalum”uliotamkwa zaidi kwa ajili ya Matengenezo ulikuwa Ushuhuda uliotolewa na watawala Wakristo wa Ujeremani huko kwa baraza la Spires mwaka 1529. Uhodari na msimamo wa watu wale wa Mungu vikaimarisha uhuru wa zamiri kwa karne zilizofuata, na wakatoa kwa kanisa lililotengenezwa jina la Protestanti.TSHM 91.1

  Maongozi ya Mungu yakazuia nguvu zilizopinga ukweli. Charles Quint akakusudia kuangamiza Matengenezo, lakini mara kwa mara alipoinua mkono wake kwa kupinga akalazimishwa kugeukia kando ya pigo. Tena na tena kwa wakati wa hatari majeshi ya Turki valipotokea kwa mpaka, ao mfalme wa Ufransa ao Papa mwenyewe alifanya vita kwake. Kwa hiyo miongoni ya vita na fujo ya mataifa, Matengenezo yakapata nafasi ya kujiimarisha na kujipanua.TSHM 91.2

  Lakini, wakati ukafika ambao wafalme wakatoliki wakafanya tendo la umoja juu ya kupinga Watengenezaji. Mfalme akaitisha baraza kukutanika huko Spires munamo mwaka 1529 na kusudi la kuharibu upingaji wa imani ya dini. Kama mpango huo ukishindwa kwa njia ya imani Charles alikuwa tayari kutumia upanga.TSHM 91.3

  Wakatoliki huko Spires wakaonyesha uadui wao kwa wazi juu ya Watengenezaji. Akasema Melanchton: “Tunakuwa maapizo na takataka ya ulimwengu; lakini Kristo atatazama chini kwa watu wake maskini, na atawalinda.” Watu wa Spires wakawa na kiu cha Neno la Mungu, na, ingawa kulikuwa makatazo, maelfu wakakutanika kwa huduma iliyofanywa ndani ya kanisa ndogo la mchaguzi wa Saxony. Jambo hili likaharakisha shida. Uvumilivu wa dini ukaimarishwa kwa uhalali, na vikao vya injili vikakusudia kupinga uvunjaji wa haki zao. Luther hakuruhusiwa kuwa Spires lakini pahali pake pakatolewa kwa wafuasi wake na watawala ambao Mungu aliinua kwa kutetea kazi yake. Frederic wa Saxony akatengwa na kifo, lakini Duke Jean, muriti wake (aliyemfuata), akakaribisha kwa furaha Matengenezo na akaonyesha uhodari mkubwa.TSHM 91.4

  Mapadri wakadai kwamba taifa ambalo lilikubali Matengenezo liwe chini ya mamlaka ya Warumi. Watengenezaji kwa upande mwengine, hawakuweza kukubali kwamba Roma ilipashwa tena kuleta mataifa yale chini ya utawala wake yale yaliyopokea Neno la Mungu.TSHM 91.5

  Matengenezo haikuanzishwa bado, Amri ya Worms ilipaswa kutumiwa kwa nguvu; na kwamba “Mahali ambapo watu hawangeweza kuilazimisha bila hatari ya uasi, hawakupasa kuingiza matengenezo mapya, ... hawakupashwa kupinga ibada ya misa, hawakupashwa kuruhusu mkatoliki wa Roma kukubali dini ya Luther.” Shauri hili likakubaliwa katika baraza, kwa kutoshelewa ukubwa kwa mapadri na maaskofu.TSHM 92.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents