Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Luther Anaamuriwa Kufika Barazani

    Baraza sasa likaomba kuonekana kwa Mtengenezaji. Mwishowe mfalme akakubali, na Luther akaalikwa. Mwito ukafwatana na ruhusa ya kusafiri salama. Hati hizo mbili zikapelekwa Wittenberg na mjumbe aliyeagizwa kumusindikiza Worms.TSHM 67.3

    Kujua chuki na uadui juu yake, rafiki za Luther waliogopa kwamba cheti cha kusafiri salama hakitaheshimiwa. Akajibu: “Kristo atanipa Roho yake kwa kushinda wahuduma hawa wa uongo. Nina wazarau katika maisha yangu; nitawashinda kwa kifo changu. Huko Worms wanashugulika sana kwa kunilazimisha; ni kane kukana kwangu kutakuwa huku: Nilisema zamani kwamba Papa alikuwa kasisi wa Kristo; sasa na tangaza kwamba yeye ni mpinzani wa Bwana, na mtume wa Shetani.”TSHM 67.4

    Zaidi ya mjumbe wa mfalme, rafiki watatu wakakusudia kumsindikiza Luther. Moyo wa Melanchton ukaambatana kwa moyo wa Luther, na akatamani sana kumfuata. Lakini maombi yake yakakataliwa. Akasema Mtengenezaji: “Kama sitarudi, na adui zangu wakiniua, endelea kufundisha, na kusimama imara katika ukweli. Utumike kwa nafasi yangu. ... Kama ukizidi kuishi, mauti yangu itakuwa ya maana kidogo.”TSHM 67.5

    Mioyo ya watu ikagandamizwa na maono ya huzuni. Waliambiwa kwamba maandiko ya Luther yalihukumiwa huko Worms. Mjumbe, huogopa kwa ajili ya usalama wa Luther kwa baraza, akauliza kama alikuwa akiendelea kutamani kwenda. Akajibu: “ijapokuwa nilikatazwa katika kila mji, nitaendelea.”TSHM 68.1

    Huko Erfurt, Luther akapitia katika njia alizokuwa akipitia kila mara, akazuru kijumba chake cha nyumba ya watawa, na akafikiri juu ya mapigano ambamo nuru iliojaa sasa katika Ujeremani imetawanywa juu ya roho yake. Akalazimishwa kuhubiri. Jambo hili alikatazwa kulifanya, lakini mjumbe akamtolea ruhusa, na mtu aliyefanywa zamani mtu wa kazi ngumu za nyumba ya watawa, sasa akaingia kwa mimbara.TSHM 68.2

    Watu wakasikiliza kwa kushangaa sana. Mkate wa uzima ulivunjwa kwa roho hizo zenye njaa. Kristo aliinuliwa mbele yao na juu ya wapapa, maaskofu, wafalme (wakuu), na wafalme. Luther hakusema juu ya maisha yake katika hatari yake. Katika Kristo alikuwa amejisahau mwenyewe. Akajificha nyuma ya Mtu wa Kalvari, akitafuta tu kuonyesha Yesu kama Mkombozi wa wenye zambi.TSHM 68.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents