Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Maelfu ya Wachungaji (Pasteurs) Walifukuzwa

  Katika karne ya kumi na saba maelfu ya wachungaji walifukuzwa na watu wakakatazwa kuhuzuria mikutano yo yote ya dini isiyokuwa ile iliyoruhusiwa na kanisa. Ndani ya kimbilio la vilindi mwituni, wale watoto wa Bwana walioteswa walikusanyika kwa kumimina roho zao katika maombi (sala) na kusifu. Wengi waliteseka kwa ajili ya imani yao. Gereza zilijaa, jamaa zikatengana. Lakini mateso hayakunyamazisha ushuhuda wao. Wengi walilazimishwa kuvuka bahari kwenda Amerika na hapo ndipo paliwekwa msingi wa utaalamu na uhuru wa dini.TSHM 117.5

  Ndani ya gereza kulijaa na watu waliofanya makosa makubwa, John Bunyan, akapumua hewa ya mbinguni na akaandika mizali yake ya ajabu ya safari ya msafiri kutoka kwa inchi ya uharibifu kwenda kwa mji wa mbinguni. Pilgrim’s Progress [Maendeleo ya Msafiri] na Grace Abounding to the Chief of Sinners [Neema nyingi kwa mkuu wa wenye zambi] vimeongoza nyayo nyingi kwa njia ya uzima.TSHM 118.1

  Katika siku ya giza ya kiroho Whitefield na Wesleys wakatokelea kama wachukuzi wa nuru kwa ajili ya Mungu. Chini kanisa lililoanzishwa watu wakarudia zambini ambayo ni vigumu kutofautisha kwa ushenzi. Watu wa vyeo vya juu wakacheka uchaji wa Mungu; watu wa vyeo vya chini wakazamishwa kwa maovu. Kanisa halikuwa na uhodari ao imani kwa kusaidia maanguko ya neno la kweli.TSHM 118.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents