Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kushambulia Ufalme wa Shetani

  Ujumbe wa Wavaudois kwa uangalifu ukatoa sehemu zilizoandikwa kwa uangalifu za Maandiko matakatifu. Nuru ya ukweli ikaingia kwa akili nyingi za giza, hata Jua la Haki likaangaza katika moyo nyali zake za kupenya. Kila mara msikilizaji alihitaji sehemu ya Maandiko ipate kukaririwa, kana kwamba apate kuhakikisha kwamba alisikia vizuri.TSHM 27.1

  Wengi waliona ni bure namna gani uombezi wa watu kwa ajili ya wenye zambi hauna faida. Wakapiga kelele kwa furaha, “Kristo ni kuhani wangu; damu yake ni kafara yangu; mazabahu yake ni mahali pangu pa kuungamia”. Ilikuwa mufuriko mkubwa wa nuru uliyo kuwa juu yao, hata walionekana kwao kwamba walichukuliwa mbinguni. Hofu yote ya kifo ikafutika. Sasa waliweza kutamani gereza kama wangeweza kwa hiyo kutukuza Mkombozi wao.TSHM 27.2

  Katika mahali pa siri Neno la Mungu lililetwa na kusomwa, mara zingine kwa roho moja, wakati mwingine kwa kundi ndogo la watu lililotamani sana nuru. Mara nyingi usiku mzima ulitumiwa kwa namna hii. Mara kwa mara maneno kama haya yakasemwa: “Je, Mungu atakubali sadaka yangu? Atanifurahia? Atanisamehe”? Jibu lilikuwa, soma, “Kujeni kwangu, ninyi wote munaosumbuka na wenye mizigo mizito, nami nitawapumzisha ninyi”. Matayo 11:28.TSHM 27.3

  Roho zile zenye furaha zikarudia nyumbani mwao kutawanya nuru, kukariri kwa wengine, kwa namna walivyoweza, maarifa mapya yao. Walipata ukweli na njia ya uhai! Maandiko yalisemwa kwa mioyo ya wale wanaotamani ukweli.TSHM 27.4

  Mjumbe wa ukweli alikwenda kwa njia yake. Kwa namna ninyi wasikilizaji wake hawakuuliza alitoka wapi ao alikwenda wapi. Walikuwa wamekwisha kupatwa na ushindi kwa hiyo hawakuwa na wazo kwa kumuuliza. Aliweza kuwa malaika kutoka mbinguni! Walitaka maelezo zaidi juu ya jambo hilo.TSHM 27.5

  Katika mambo mengi mjumbe wa ukweli alifanya njia yake kwa inchi nyingine ao alikuwa akipunguza maisha yake katika gereza ao labda mifupa yake iligeuka nyeupe mahali aliposhuhudia ukweli. Lakini maneno aliyoacha nyuma yalikuwa yakitenda kazi yao.TSHM 27.6

  Waongozi wa Papa waliona hatari kutoka kwa kazi za hawa watu wanyenyekevu wa kuzunguka zunguka. Nuru ya ukweli ingefutia mbali mawingu mazito ya kosa lililofunika watu; ingeongoza akili kwa Mungu peke yake na mwisho kuharibu mamlaka ya Roma.TSHM 27.7

  Watu hawa, katika kushika imani ya kanisa la zamani, ilikuwa ni ushuhuda imara kwa uasi wa Roma na kwa hivyo ikaamsha chuki na mateso. Kukataa kwao kwa kuacha Maandiko ilikuwa ni kosa ambalo Roma haikuweza kuvumilia.TSHM 28.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents