Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kuhesabiwa Haki kwa Imani

  Mafundisho makubwa ya kuhesabiwa haki kwa imani, yaliyofundishwa wazi wazi na Luther, yalikuwa karibu kusahauliwa kabisa; kanuni ya kanisa la Roma ya kutumaini matendo mema kwa ajili ya wokovu yakakamata nafasi yake. Whitefield na Wesleys wawili walikuwa watafuti wa kweli kwa ajili ya wema wa Mungu. Hii walifundishwa kuwekwa salama kwa njia ya wema na kushika maagizo ya dini.TSHM 118.3

  Wakati Charles Wesley kwa wakati moja alipopata ugonjwa na akatumaini kwamba kifo kilikuwa karibu, akaulizwa, msingi wa tumaini lake la uzima wa milele ulikuwa juu ya kitiu gani. Jibu lake: “Nimetumia juhudi yangu bora kumtumikia Mungu.” Rafiki ilionekana hakutoshelewa kabisa kwa jibu hili. Wesley akafikiri: “Nini! ... Anatamani kuninyanganya juhudi yangu? Sina kitu kingine cha kutumainia.” Hiyo ndiyo ilikuwa giza ambayo iliyoimara kwa kanisa, kugeuza watu kutoka kwa tumaini lao pekee la wokovu--damu ya Mkombozi aliyesulubiwa.TSHM 118.4

  Wesley na washiriki wake wakaongozwa kufahamu kwamba sheria ya Mungu inafikishwa mawazoni pia kwa maneno na matendo. Kwa juhudi za kazi na maombi wakafanya bidii ya kushinda maovu ya moyo wa asili. Wakaishi maisha ya kujinyima na kujishusha, wakachunguza kwa uaminifu kila mpango waliochukua ambao ungeweza kuwa wa kusaidia kwa kupata utakatifu ule ambao uliweza kutunza wema wa Mungu. Lakini juhudi zao wenyewe hazikuweza kuwapa uhuru kutoka kwa hukumu ya zambi ao kuvunja uwezo wake.TSHM 118.5

  Mioto ya ukweli wa Mungu, ambayo ilikuwa karibu kuzimika juu ya mazabahu ya dini ya Kiprotestanti, ilipashwa kuwashwa kutoka kwa mwenge wa zamani uliotolewa na Wakristo wa Bohemia. Wengine miongoni mwao, wakapata kimbilio katika Saxe (Saxony), wakalinda imani ya zamani. Kutoka kwa Wakristo hawa nuru ikaja kwa Wesley.TSHM 119.1

  Yohana na Charles wakatumwa kwa ujumbe kuenda Amerika. Katika meli kulikuwa na kundi la waMoravians. Wakakutana na zoruba kali sana, na Yohana, akawa uso kwa uso na kifo, akajisikia kwamba hakuwa na hakikisho la amani na Mungu. Lakini Wajeremani wakaonyesha utulivu na kutumaini kwamba alikuwa mgeni. “Tangu zamani,” akasema, “nilichunguza umuhimu mkuu wa mwenendo (tabia) wao. ... Wakawa sasa na bahati ya kujaribu kwamba walikuwa huru bila mafikara ya woga pia na ile ya kutokuwa na kiburi, hasira na kulipisha kisasi. Katikati ya zaburi kwa kazi yao ilianza, bahari ikapasuka, na kupasua tanga kubwa kwa vipande vipande, ikafunika merikebu, na kumwanga kati kati ya sakafu kana kwamba kilindi kikuu kimekwisha kutumeza. Kilio cha nguvu kikaanza miongoni mwa Waingereza. Wajeremani kwa utulivu wakaendelea kuimba. Nikauliza mmojawapo wao baadaye,`Hamkuwa na hofu? ‘ Akajibu Namshukuru Mungu, hapana.’ Nikauliza, `Lakini wake wenu na watoto hawakuwa na hofu?’ Akajibu kwa upole, `Sivyo; wake wetu na watoto hawaogopi kufa.’”TSHM 119.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents