Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ngurumo ya Laana

  Laana za Papa zikanguruma juu ya Geneve. Namna gani mji huu mdogo ulishindana na mamlaka hodari ya kanisa ambalo lilitetemesha wafalme na watawala kutii?TSHM 108.1

  Kushinda kwa kwanza kwa Matengenezo kukapita, Roma ikakusanya nguvu mpya kwa kutimiza maangamizi yake. Amri ya WaJesuite ikaanzishwa, kali zaidi, ya tabia mbaya, na hodari kuliko washujaa wote wa Papa. Hawakujali upendo wa kibinadamu, na zamiri yote ikanyamazishwa, hawakujali amri, upendo, lakini ile ya agizo lao. (Tazama mwisho wa kitabu.)TSHM 108.2

  Injili ya Kristo iliwezesha wafuasi wake kuvumilia mateso, bila kukatishwa tamaa na baridi, njaa, kazi ngumu na umaskini, kushindania kweli machoni pa mbao (zenye vyango) za kutundikia, gereza, na kigingi. Kijesuitisme kikatia wafuasi wake moyo mamlaka ya kweli silaha zote za udanganyifu. Hawakuogopa kufanya kosa kubwa ao kutumia uwongo wa haya, kwao kujigeuza sura kwa uwongo haikuwa taabu. Ilikuwa shabaha yao waliyojifunza kukomesha dini ya Kiprotestanti na kuimarisha utawala wa Papa.TSHM 108.3

  Walivaa vazi la utakatifu, wakizuru nyumba za gereza na mahospitali, kusaidia wagonjwa na maskini, na kuchukua jina takatifu la Yesu, aliyekwenda akifanya matendo mema. Lakini chini ya umbo la inje lisilo na kosa, makusudi mabaya na ya uuaji yalikuwa yakifichwa.TSHM 108.4

  Ilikuwa kanuni ya asili ya amri kwamba “mwisho huthibitisha njia. Uongo, wizi, ushuhuda wa uongo, mauaji ya siri, yaliruhusiwa yalipotumiwa kwa faida ya kanisa. Kwa siri Wajesuite walikuwa wakiingia ndani ya maofisi ya serkali nakupanda juu, kuwa washauri wa mfalme na kuongoza mashauri ya mataifa. Wakajifanya watumishi kwa kupeleleza mabwana wao. Wakaanzisha vyuo vikubwa kwa ajili ya watoto wa watawala na watu wakuu, na vyuo kwa ajili ya watu wote. Watoto wa wazazi wa Kiprotestanti kwa njia ya vyuo hivyo walikuwa wakivutwa kushika kanuni za kanisa la Papa. Kwa hivyo uhuru ambao mababa zao walikuwa wakishindania na kutoka damu ukasalitiwa na watoto wao. Po pote, Wajesuites walipokwenda, kukafuata mwamsho wa mafundisho ya kanisa la Papa.TSHM 108.5

  Kwa kuwapatia uwezo mwingi, tangazo la Papa likatolewa kwa kuimarisha (“Inquisition”) (Baraza kuu la kuhukumia wapinga ibada ya dini la Papa. Mahakama haya ya kutisha yakawekwa tena na wajumbe wa kanisa la Roma, na mambo mabaya ya kutisha kwa kuweza kuonyeshwa mchana yakakaririwa ndani ya gereza za siri (cachots). Katika inchi nyingi maelfu na maelfu ya watu--wa faida kuu kwa taifa, wenye elimu sana na waliojifunza zaidi, waliuawa ao kulazimishwa kukimbilia kwa inchi zingine. (Tazama Nyongezo.)TSHM 109.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents